AMECEA PLENARY 2022

July 8, 2022 - July 19, 2022
Loading Events
  • This event has passed.

AMECEA

AMECEA ni kifupi cha “Association of Member Episcopal Conferences in Eastern  Africa” ni Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya nchi nane  za Afrika Mashariki na Kati ambazo ni

  1. Ethiopia(1979),
  2. Eritrea(1993),
  3. Kenya(1961),
  4. Malawi(1961),
  5. Tanzania(1961),
  6. Zambia(1961),
  7. Sudan(1979) na
  8. Uganda(1961).
  9. Somalia(1995) na Jibuti (2002) ni watazamaji.

Shirikisho hilo lilianzishwa mwaka 1961 na Makao makuu ya AMECEA yako Nairobi nchini Kenya.

MWANZO WA AMECEA

  • AMECEA (wakati huo Inter-Territorial Episcopal Board in Eastern Africa ITEBEA) ilikuwa chimbuko la Maaskofu wa Kikatoliki wa Tanganyika (Tanzania ya leo).
  • Mnamo 1960 walipendekeza, kupitia Ujumbe wa Kitume wa wakati huo (Nunciature ya leo) huko Nairobi, kwamba kuwe na ushirikiano kati ya Maaskofu wa Kikatoliki katika eneo hilo.
  • Wakati huo nchi zifuatazo zilikuwa chini ya Ujumbe wa Kitume wa Nairobi ambao ni Kenya, Nyasaland (Malawi ya leo), Uganda, Sudan, Tanganyika na Northern Rhodesia (Zambia ya leo).
  • Mabaraza haya mengine ya Maaskofu yalipokubali ulazima wa kufanya kazi pamoja, Mjumbe wa Kitume wa wakati huo (Nuncio wa leo) Monsinyo Guido Del Mestri alishauriana na Roma. Roma ilitoa kibali chake.

 

Sababu za Mshikamano

KANISANI na Mtaguso wa Vatikani II

  • Katika Kanisa Mahalia wakati huo kulikuwa na upepo wa mabadiliko katika Kanisa na jamii katika eneo hili.
  • Katika kipindi hicho mapadre wengi zaidi wa Kiafrika katika majimbo walikuwa wakiwekwa wakfu na wengine wakipewa mafunzo nje ya nchi.
  • Maaskofu wa Kiafrika walikuwa tayari wamejitokeza ambao ni Maaskofu Kiwanuka (Uganda), Kardinali Otunga, (Kenya), Chitsulo (Nyasaland) na Kardinali Rugambwa, wa (Tanganyika).
  • Kanisa lilikuwa tayari likipitia mabadiliko kutoka kuwa la kimisionari hadi Kanisa mahalia. Na kipindi cha mpito, kama tunavyojua, mara nyingi ni cha kusisimua.
  • Maswali ambayo yaliwasumbua Maaskofu katika eneo hilo, ambao wengi wao walikuwa wamisionari, ni pamoja na:
  • Je, Kanisa lililazimika kujitayarishaje kwa ajili ya mabadiliko yasiyoepukika ambayo Vatikani ya Pili ilikuwa ikianzisha?
  • Je, makasisi wa Kiafrika walikuwa wamejitayarisha vya kutosha kulichukua na kuliendesha Kanisa kwa mafanikio na kwa uhakika?

Kwa hiyo kulikuwa na hisia za kujishughulisha na vilevile woga na wasiwasi kwa upande wa wamisionari ambao wakati wao, waliamini, ulikuwa unakwisha.

KATIKA JAMII

Kipindi cha Uhuru

  • Tanganyika (1961), Uganda (1962), Kenya (1963), Nyasaland (1964) na Northern Rhodesia (1964) zote zilipata Uhuru hivi karibuni chini ya viongozi mahiri kama vile Hastings Kamuzu Banda (Nyasaland), Kenneth Kaunda (Northern Rhodesia), Jomo Kenyatta (Kenya), Julius Kambarage Nyerere (Tanganyika) na Milton Obote (Uganda).
  • Kanisa kwa ujumla liliwashuku wengi wao kuegemea ukomunisti na ujamaa (atheistic socialism) uliokuwa haumwamini Mungu. Kwa hiyo Maaskofu walihofia mustakabali wa Kanisa na taasisi zinazohusiana na Kanisa (kama vile shule) katika Afrika kwa ujumla na hasa katika eneo hili.
  • Vyuo vikuu kama vile Makerere vikifuatiwa na Nairobi na Dar-es-Salaam vilikuwa vimeanzishwa tayari.
  • Viongozi wa kisiasa na wa kiraia wanaokuja mara nyingi walikuwa bidhaa za vyuo hivi na vingine vya ng’ambo. Na Kanisa Katoliki hadi wakati huo lilikuwa limefanya vyema katika elimu ya msingi na vyuo vya ualimu. Lilikuwa bado halijajitosa katika elimu ya vyuo vikuu.
  • Maandishi yaliyotolewa, yalikuwa yakisema kwamba ilikuwa ni wakati muafaka kwa Kanisa kufanya hivyo. Jamii ilihitaji viongozi wanaoongozwa na maadili. Viongozi ambao walikuwa na sifa za juu na wabunifu, lakini wakati huo huo ambao walikuwa watu wa uadilifu wa maadili wakiongozwa na maadili ya Kikristo na injili.
  • Yote haya yalipelekea kuwa na chombo cha pamoja kitakachoweza kuyaratibisha; na hapo ndipo ikazaliwa AMECEA.

Mkutano wa kwanza: Julai, 1961

Mkutano wa kwanza ulifanyika jijini Dar es Salaam tangia Tarehe 17-26 Julai, 1961 chini ya Kauli mbiu “Uhai wa Kanisa ndani ya Afrika” (The Future of the Church in Africa).

Agenda za Mkutano huo:

  • Kanisa na Vyombo vya Mawasiliano: TV, vituo vya matangazo ya reddio na viwanda vya uchapishaji.
  • Malezi ya Kiroho kwa mapadre wa majimbo.
  • Hitaji la kuwa na kituo cha maboresho ya Uchungaji na malezi endelevu.
  • Uwezekano wa kuwa na Chuo Kikuu kimoja kinachounganisha nchi za AMECEA.
  • Mpango mkakati wa kuwa na Elimu ya Kujitegemea
  • Maendeleo ya shule za kikatoliki na Elimu ya Ukatoliki (Hitaji la kuwa na mtaala wa somo la dini/ a Christian religious education syllabus).
  • Masuala yote yanayohusu Haki na Amani katika eneo husika.

 

AMECEA inajiandaa na Mkutano wake 2022 kuhusu “ekolojia fungamani”

  • Katika maandalizi ya Mkutano wa AMECEA 2022 utakaofanyika nchini Tanzania,mada iliyochaguliwa ni “Ekolojia Fungamani “ ambapo waratibu wa kitaifa wa Caritas na Tume ya Haki na Amani wa Mabaraza ya maaskofu wamezindua utafiti juu ya matokeo ya Waraka wa Laudato si’ kuhusu maendeleo endelevu na fungamani.
  • Mkutano huo wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki (AMECEA) utakaofanyika mnamo mwaka 2022 utajikita kwenye mada ya Ekolojia na utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja. (“Nurturing our Common Home: Living Laudato Si’ Towards Enhancing Integral Human Development in AMECEA Region”).
  • Ni mkutano unaowashirikisha maaskofu wa Eritrea, Ethiopia, Kenya, Malawi, Sudan, Tanzania, Uganda na Zambia. Mkutano huo utafanyika nchini Tanzania. Utafiti huo unakusudia kuandaa mwongozo wa kuhamasisha jumuiya za Wakatoliki mahalia, kuhusu mambo yaliyomo kwenye Waraka wa Papa Francisko wa “Laudato Si”.
  • Lengo kubwa la kufanya utafiti na watu wengine wa nchi mbali mbali za Kanda ya AMECEA ni kutaka kuelewa ni kitu gani wanajua kuhusu waraka wa “Laudato Si”,
  • Nini wanafikiria juu yake na nini kimefanywa au kinahitajika kufanywa ili kutekeleza mapendekezo yake.
  • Njia iliyochaguliwa ni kuona, kujadili na kutenda kulingana na matokeo ya utafiti.
  • Kwa maana hiyo Waratibu wa Haki na Amani watatathmini uchapishaji wa mwongozo wa katekesi na muhtasari rahisi wa “Laudato Sì”. Wazo pia ni kuwashirikisha wanateolojia ili utafiti uweze kuwa na msimamo wa kichungaji zaidi.
  • Mkutano huo utaangazia umuhimu wa kukuza uelewa pia wa maoni ya umma ya Kiafrika juu ya uharaka wa uongofu wa mazingira, hasa juu ya ulinzi wa bioanuwai, unyonyaji endelevu wa maliasili na juu ya umuhimu wa kuhakikisha maji na hewa safi kwa wote katika wakati muhimu na kwa mustakabali wa ubinadamu ambao una hatari ya kujiangamiza.

Tanbihi: Ikumbukwe kuwa Mkutano uliopita wa AMECEA ulifanyika mnamo Julai 2018 huko Addis Ababa, Ethiopia, kwa kuoongozwa na kaulimbiu: “Utofauti wa kupendeza, utu sawa na umoja wa amani katika Mungu” ambapo ulizungumzia mizozo inayoendelea ya kikabila na kidini katika kanda za Afrika mashariki.

 

Details

Start:
July 8, 2022
End:
July 19, 2022

Organiser

TEC
Phone
+255754624572
View Organiser Website