SALA YA KUOMBEA SINODI YA MAASKOFU:

SALA YA KUOMBEA SINODI YA MAASKOFU:

Tunasimama mbele yako Ewe Roho Mtakatifu,

Tunapokusanyika pamoja kwa Jina lako.

 

Wewe pekee unayetuongoza,

Weka maskani yako ndani ya nyoyo zetu;

Utufundishe njia ya kupita

na jinsi ya kuenenda.

 

Sisi ni dhaifu na wenye dhambi;

Usiruhusu tuendelee kuchochea machafuko.

Usiruhusu ujinga utuongoze kwenye njia mbaya,

wala utepetevu usiathiri matendo yetu.

Utuwezeshe tusisababishe machafuko.

Ujinga usituingize kamwe kwenye njia mbaya,

au utepetevu kuathiri matendo yetu.

 

Utuwezeshe ndani Yako tuwe na umoja

ili tuweze kusafiri pamoja hadi uzima wa milele,

wala tusipotee mbali kutoka njia ya kweli

 na iliyo sahihi.

 

Tunaomba hayo yote,

Kwako Wewe ufanyae kazi kila mahali na kila wakati,

 katika ushirika wa Baba na Mwana,

milele na milele,

Amina.