UMEBATIZWA NA UNATUMWA KWENDA KUTANGAZA INJILI, MWEZI OCTOBA 2019 MWEZI PEKEE WA UMISIONARI.

UMEBATIZWA NA UNATUMWA KUTANGAZA INJILI.

Mambo muhimu ya kuzingatia katika kuuishi mwezi mzima wa pekee wa Kimisionari:

 1. Kila mtu binafsi ajitahidi kukutana na Yesu Kristo anayeishi katika Kanisa lake: Katika Ekaristi Takatifu, katika Neno la Mungu, na katika Sala binafsi na ya kijumuiya. Ili kutimiza azma hii, kila parokia inaalikwa
 • kila juma iwe ina Ibada ya kuabudu (Perpetual adoration)
 • Kuwahimiza waamini kuwa na moyo wa Ibada
 • Kuhudhuria Misa za Dominika, na sikukuu zilizoamriwa
 • Kuungama mara kwa mara
 • Watu walio na vizuizi wajitahidi kuondoa vizuizi vyao ili waanze kupokea sakramenti mbalimbali.  
 • Mapadri wawe karibu na waamini katika kutoa huduma za kichungaji na kiroho
 • Watu wajipangie ratiba ya Sala na waizingatie
 • Wawepo viongozi wa sala ndani ya familia na kwenye Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo.
 1. Ushuhuda: Kila mtu ajitahidi kutafakari na kuishi ushuhuda wa Watakatifu Wamisionari, Wafiadini (Mashahidi) na Waungama imani kwani wao ni taswira ya kujipambanua na Kanisa lililoenea duniani kote.
 2. Malezi ya Umisionari: Waamini washiriki kutoa malezi ya kimisionari Kibiblia, Kikatekisimu, Kiroho na Kiteolojia. Ili kutimiza hili yafuatayo yafanyike: 
 • Kila familia inunue na kusimika Biblia. Upangwe muda wa kusoma Biblia. Kuwe na utamaduni wa kusoma  na kutafakari Neno la Mungu kibinafsi na kijumuiya.
 • Yatolewe mafundisho ya Biblia katika shule za msingi, sekondari na vyuo.
 • Biblia zipatikane kirahisi  
 • Mafundisho ya Katekisimu yatiliwe mkazo
 • Mafundisho mengine ya dini yapewe muda wa kutosha
 • Watoto waandaliwe vizuri kabla ya kupokea Ekaristi na Kipaimara
 1. Kipindi cha Ukatekumeni kiwe cha Kutosha Upendo wa Kimisionari. Waamini wajitoe kuhubiri Injili, wasaidie Uinjilishaji hasa kwa kuwa wakarimu kwa Baba Mtakatifu. Wafanye matendo ya huruma katika ngazi ya Parokia. Wawasaidie wahitaji; wasaidie Uinjilishaji wa Kanisa mahalia, n.k.
 2. Waamini wanaalikwa kusali Rozari ili kuombea mahitaji yao wenyewe na kazi ya Umisionari.
 3.  Kila taifa au Jimbo linaalikwa liwe na maadhimisho ya uzinduzi  wa Mwezi wa Pekee  wa Kimisionari, vivyo hivyo na maadhimisho ya kufunga Mwezi wa Pekee wa Kimisionari.
 4. Waamini wote wanaalikwa kuinunua, kuisoma na kuitafakari Barua ya Maximum Illud. Waitafakari waone kwa sababu gani Baba Mtakatifu ametangaza mwezi wa pekee kwa ajili ya barua hii ya Kichungaji.
 5. Waamini wafanyie kazi mapendekezo yaliyotolewa katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania.
 6. Waamini wafanyie kazi mafundisho ya familia yanayotolewa na barua ya Kwaresma ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania 2019.
 7. Waamini wanakumbushwa kufanya mafungo, hija za Parokia, Vyama vya Kitume na Majimbo. Wajumbe wafundishwe mada ya umuhimu wa Ekaristi, malezi ya Umisionari, familia, ushuhuda unaotolewa na Watakatifu na Upendo wa Kimisionari.
 8. Katika Mwezi wa Kumi wa Pekee wa Kimisionari waamini wanaalikwa kwa namna ya pekee kutoa kwa Ukarimu kwa ajili ya Baba Mtakatifu ili kumsaidia katika Uinjilishaji.
 9. Kusimika Shirika la Umoja wa Kimisionari, kitaifa (Pontifical Missionary Union)
 10. Mazoezi kiroho yafanyike kadiri ya mazingira kama vile kutembeza Msalaba nyumba hadi nyumba au kutembeza Biblia nyumba hadi nyumba.
 11. Uchumba sugu, utoaji mimba na kwenda kwa waganga wa kienyeji kupiga ramli vipigwe vita.

MAELEZO YA LOGO / NEMBO

Logo ya mwezi wa pekee wa Umisionari ina msalaba unaozunguka dunia nzima. Ukionesha ushindi wa Kristo mfufuka. Msalaba ni alama ya muungano wa Mungu na mwanadamu, na pia inaonyesha umoja wa Utume walionao. Kwa kupitia rangi zinazongÔÇÖara ni alama ya Ushindi na Ufufuko wa Kristo.

Katika Logo hii, dunia inaonekana kama inapitisha mwanga (transparent) ikiashiria kuwa Uinjilishaji hauna mipaka katika dunia nzima. Hili ni tunda la Roho Mtakatifu. Upendo wa Kikristo na Ulimwengu ambao unamiminiwa Roho unaondoa umbali na kufungua upeo wa Roho na mioyo. Maneno; ÔÇ£Umebatizwa na KutumwaÔÇØ ambayo yapo katika logo yanaonesha tabia ya kila mkristo ya ÔÇ£Ubatizo na kutangaza InjiliÔÇØ

 

Msalaba huu wa Kimisionari una rangi tano.

Rangi hizi zinawakilisha Mabara matano kama ifuatavyo:

 • Rangi nyeupe inawakilisha Bara la Ulaya
 • Rangi nyekundu inawakilisha Amerika ya Kaskazini na Kusini
 • Rangi ya kijani inawakilisha Bara la Afrika
 • Rangi ya njano inawakilisha Bara la Asia
 • Rangi ya bluu inawakilisha maeneo ya Oceania / Australia

Rangi hizi zipo katika Rozari ya Kimisionari

Rangi nyekundu inakumbusha mashahidi wa Imani wa Amerika na mbegu ya maisha mapya ya Imani ya Kikristo.

Rangi ya njano inaonesha hali ya uhai na ni ishara ya ustawi, kuzaa matunda, ujana na nguvu na pia ni rangi ya matumaini ambayo ni moja ya fadhila kuu za Kikristo (theological virtues)

Rangi nyeupe ni alama ya furaha na ya  kuanza maisha mapya katika Kristo. Hii ni changamoto kwa bara la Ulaya, ili liweze kupata nguvu na kuanza upya kazi ya uinjilishaji kutokana na mchango uliotolewa na makanisa na watakatifu waliotoka bara hilo.

Njano ni rangi ambayo inaonesha maji ya uzima ambayo yanatuliza kiu yetu na kuturejesha kwenye njia iendayo kwa Mungu. Pia ni rangi inayoonesha Mbingu ambayo ni alama ya kuonesha kuwa Mungu anaishi miongoni mwetu.

 

Kaulimbiu: Umebatizwa na Unatumwa kutangaza Injili

Add new comment

Restricted HTML

 • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
 • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.