UJUMBE WA BABA MTAKATIFU KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA WAGONJWA DUNIANI FEBRUARI 11, 2019

ÔÇ£MLIPOKEA BILA MALIPO, TOENI BILA MALIPOÔÇØ (MT.10:8)

 

Wapendwa Kaka na dada zangu,

ÔÇ£Mlipokea bila malipo, toeni bila malipoÔÇØ(Mt 10:8). Hayo ni maneno yaliyotamkwa na Yesu Kristu alipowatuma mitume wake kwenda kueneza Injili,ili ufalme wake uweze kuenea kupitia matendo ya ukarimu na upendo.

 

Mlipokea bila malipo, toeni bila malipo (Mt 10:8).

Katika kuadhimisha Siku ya Wagonjwa Duniani, itakayoadhimishwa rasmi tarehe 11-2-2019 huko Calcutta, India, Kanisa- kama Mama kwa watoto wake wote, na hasa walio wagonjwa, linatukumbusha kuwa ishara ya ukarimu na upendo kama wa yule Msamaria Mwema kama njia thabiti ya Uinjilishaji. Kuwajali na kuwatunza wajonjwa inahitaji utaalamu, upole, unyoofu na unyenyekevu unaotolewa bila kujibakiza, matunzo yanayomfanya yule anaye hudumiwa kuonja kupendwa.

 

Maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu.Mt. Paulo anauliza ÔÇ£ Ni kitu gani ulicho nacho ambacho hukupokea? (Kor. 4:7). Ni ukweli na dhahiri kabisa kwa sababu ulicho na ulichonacho ni zawadi, maisha ya mwanadamu hayawezi kufanywa kuwa ni mali binafsi ya mtu na hasa kwa sasa kutokana na kukua kwa sayansi ya tiba na bioteknologia ambavyo vinaweza kutushawishi kuchezea mti wa uhai (Mw 3:24).

 

Katika utamaduni wa sasa wa kutapanya na kutojali, naomba nitamke kuwa ÔÇ£ukarimuÔÇØndilo neno lifaalo kutoa changamoto kwa tabia za sasa za ubinafsi na jamii kugawanyika; ukarimu ukihuisha upya mahusiano mapya na ushirikiano kati ya watu na tamaduni nyingine. Mazungumzano-ambayo ni chimbuko la ukarimu hufungua fursa ya mwanadamu kukua na kuvunja utengano baina ya jamii. ÔÇ£UkarimuÔÇØ ni zaidi ya kutoa zawadi inahusisha kujitoa binafsi, na siyo kuhamisha vitu au mali na kutoa kwa wengine.

 

ÔÇ£UkarimuÔÇØ.

ÔÇ£UkarimuÔÇØ hutofautiana na kutoa zawadi kwa sababu kutoa ÔÇ£zawadiÔÇØ huhitaji kujitoa binafsi. Ukarimu huchajizwa na nia ya kutaka kujenga uhusiano na yule anayepokea ukarimu/zawadi. Ni hali ya kuwakubali wengine ambayo ndio msingi wa jamii. Ukarimu ni asili ya Mungu, ukarimu wa Mungu ambao ulifikia kilele kwa ujio wa Mwanae na kushuka kwa Roho Mtakatifu.

 

Kila mmoja wetu ni maskini, mhitaji na fukara. Tunapozaliwa, tunahitaji matunzo toka kwa wazazi ili tuishi, na katika kila hatua ya maisha tunabaki wategemezi kwa watu wengine kwa kiwango fulani. Daima tunakuwa tunatambua kuhusu udhaifu wetu kama ÔÇ£viumbeÔÇØ, mbele ya watu wengine na dhaifu katika hali mbalimbalihali. Unyenyekevu wa kukubali udhaifu wetu utufanye tuone haja ya kushirikiana na wengine kama tendo la fadhila katika maisha.

 

Kuukubali ukweli huo hutufanya tutende kwa kuwajibika kwa kukuza yaliyo mema kwa mtu binafsi na kwa jamii. Ni pale tu tutakapojiona, sio kama tulio jitenga na dunia bali tulio katika maungano na wengine, tutaweza kujenga utamaduni wa  umoja unaojali dunia yetu ya pamoja.

 

Tusiogope kujiona wahitaji au wategemezi kwa wengine, kwa sababu binafsi na kwa juhudi zetu tuu hatutaweza kumaliza mapungufu yetu. Kwa hiyo tusiogope kukiri mapungufu yetu,kwa kuwa Mungu mwenyewe,kupitia Yesu Kristu alijinyenyekesha kwetu (Wafil. 2:8) na anaendelea kufanya hivyo;  na katika umaskini/udhaifu wetu anatusaidia na kutukirimu zaidi ya matarajio yetu.

 

Katika kuadhimisha rasmi siku hii nchini India, napenda kukumbusha kwa furaha na kuenzi mfano wa Mt.Teresia wa Calcutta- ambaye ni mfano wa ukarimu uliodhihirisha upendo wa Mungu kwa maskini na wagonjwa. Kama nilivyo sema wakati wa kutangazwa mtakatifu, Mama Teresa, maisha yake yote yalikuwa ni ya kumimina/kusambaza  huruma ya Mungu, akajiachia aweze kutumika kwa ajili ya wote na kuwa mtetezi wa uhai wa wale ambao hawajazaliwa na wale walioachwa na kutupwa. Alijinyenyekeza kwa walioachwa wafe kandokando mwa barabara, akiona ndani mwao hadhi na uzuri wao wa Kimungu. Alifanya sauti yake ikasikika miongoni mwa wenye mamlaka ya dunia wajitambue na wasutwe na dhamiri zao kwa maovu--maovu na umaskini walio utengeneza kwa watu wengine.

 

Kwa Mama Teresa, huruma ilikuwa chumvi iliyotoa ladha kwa kazi yake. Ilikuwa ni mwanga ulioangaza kwenye giza la wengi ambao hawakuwa tena na machozi ya kulia kutokana na umaskini na mateso. Utume wake katika miji na pembezoni mwa miji umebaki kuwa ushuhuda wa ukaribu wa Mungu kwa maskini (Homily, 4 September 2016)

 

Mtakatifu, Mama Teresa, tusaidie kuelewa kuwa kipimo cha matendo yetu kiwe upendo wa kutojibakiza kwa kila mwanadamu, bila kujali lugha, kabila au dini ya mtu. Mfano wake unaendelea kutuongoza kwa kufungua fursa za furaha na matumaini kwa wote wenye kiu ya uelewa na upendo na hasa wale wanaoteseka.

 

Ukarimu huchochea na kudumisha kazi nyingi za wahudumu wa kujitolea ambazo ni muhimu sana  katika sekta ya afya na hasa matunzo ya wagojnwa;wahudumu ambao wanawakwa na moyo wa msamaria mwema. 

 

Nitoe shukrani zangu na kutia moyo taasisi zote za wahudumu wa kujitolea waliojikita katika kuwasafirisha na kuwasaidia wagonjwa, wale wote wanao hamasisha uchangiaji wa damu na uchangiaji wa viungo vya kusaidia wengine. Huduma za kujitolea ni moja ya eneo la pekee linalodhihirisha umuhimu wa Kanisa katika utunzaji wa wagonjwa na utetezi wa haki za wagonjwa na hasa wale walio athiriwa na magonjwa yanayohitaji uangalizi maalumu. Napenda pia kutambua juhudi kubwa mnayofanya ya kujenga ufahamu na kuzuia magonjwa .Kazi yenu ya kujitolea katika vituo vya afya na nyumbani  pamoja na kutoa uangalizi na kutoa huduma za kiroho ni ya umuhimu na msingi mkubwa.

 

Wagonjwa wasiohesabika walio peke yao, wazee, waliodhaifu kiakili na kimwili wanafaidika na huduma zenu. Nawahimiza kuendelea kuwa ishara ya uwepo wa Kanisa katika dunia ya sasa. Mhudumu wa kujitolea ni rafiki mzuri ambaye mgonjwa anaweza kueleza mawazo yake na hisia zake kutokana na uvumilivu na unyenyekevu wao wa kusikiliza, voluntia anamwezesha mgojwa aache kuwa ni mpokea huduma bali mshiriki mkamilifu wa mchakato wa matibabu hali inayo rudisha matumaini na kufungua milango ya kuwa wazi ili kuboresha matibabu. Kazi ya voluntia hueneza maadili mema, matendo mema na kujenga mfumo wa kuishi ulio jikita katika misingi ya ukarimu. Ni njia nyingine ya kufanya huduma za afya ziwe ni za kibinadamu zaidi.

 

Roho ya ukarimu inapaswa kuchochea taasisi za afya za Kikatoliki iwe ziko katika nchi zilizoendelea au katika nchi maskini za dunia yetu kwa kutoa huduma zao wakiongozwa na Injili.Taasisi za Afya za Kikatoliki zinaalikwa kuwa mfano wa kujitoa, wa ukarimu na zenye mshikamano kama mwitiko dhidi ya hulka ya kutaka faida bila kujali madhara; hulka ya kutoa ili kupokea na hulka ya kunyonya bila huruma.

 

Nahimiza kila mmoja, katika ngazi zote kukuza moyo wa ukarimu na wa kuwa zawadi kwa wengine kama njia pekee ya kushinda utamaduni wa kutaka faida na utapanyaji. Taasisi za afya za Kanisa Katoliki zisitumbukie katika mtego wa kuendesha bisashara ya huduma za afya, zinapaswa kujikita katika kumhudumia mtu kuliko kuangalia faida.Tunatambua kuwa huduma za afya ni shirikishi, inayohusu kufanyakazi na wengine, inayohitaji kuaminiana, urafiki na mshikamano. Ni hazina inayofurahiwa kikamilifu pale inapotolewa kwa wengine. Furaha ya kujitoa na kuwa zawadi kwa wengine ndiyo (barometer) kipimo cha afya ya Mkristu.

 

Nawakabidhi nyote kwa Maria mfariji wa wagonjwa. Atusaidie kushirikishana karama tulizopokea kwa roho radhi ya masikilizano na kupokeana, tuishi kama kaka na dada katika Kristu tukiwa makini kutambua mahitaji ya wengine, kutoa kwa moyo wa ukarimu na kujifunza moyo wa kujitoa kwa ajili ya wengine.

 

Kwa upendo mkuu,nawahakishia ukaribu wangu nanyi katika sala na kwenu nyote nawatumia baraka za Kitume. Vatican City, 25 November 2018

Katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Kristu Mfalme wa Ulimwengu

FRANCIS - PAPA

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.