


KUMBUKUMBU KUFARIKI ASKOFU AMEDEUS MSARIKIE 2013
Leo Alhamisi ya juma la 4 la Mwaka C wa Kanisa
Tunakumbuka kwa namna ya pekee utume wa Mhashamu Amedeus Msarikie aliyekuwa Askofu wa jimbo Katoliki Moshi ambaye alifariki tarehe kama ya leo mwaka 2013.
Tunaungana na wana Jimbo Katoliki Moshi kumuombea na kumtakia Pumziko la Milele Askofu Amedeus Msarikie Apumzike kwa Amani.
Pichani ni Askofu Amedeus Msarikie( enzi za uhai wake) akiwa pamoja na Askofu Methodius Kilaini ( alipokuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Dar es salaam) Ambapo kwa sasa ni Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki Bukoba, wakiwa wameshika kitenge maalumu cha mwaka wa Rozari kilichoandaliwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, hapa walikuwa wakizindua rasmi matumizi ya kitenge hicho kwa ajili ya shunguli mbalimbali za kikanisa kwa mwaka wa Rozari, nyuma yao ni kanisa la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili lililopo TEC Kurasini Jijini Dar es salaam.
Picha na Maktaba ya Gazeti Kiongozi.