TAFAKARI YA SIKU IJUMAA YA JUMA LA 3 LA KWARESIMA MWAKA C 29.03.2019

TAFAKARI KUTOKA KATIKA INJILI YA MARKO 12:28-34.

 Tumsifu Yesu Kristu…

         Wapendwa taifa la Mungu karibuni katika tafakari fupi kutoka kwa mwinjili Marko 12:28-34. Tukiongozwa na wazo hili “sikia Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, na kwa akilli zako zote na kwa nguvu zako zote, Mpende jirani yako kama nafsi yako” (Marko 12:29-31) Mungu anatueleza juu ya mapendo kwa yeye mwenyewe na jirani zetu. Katika amri kuu ya mapendo ambayo ndio mwendelezo na mkazo wa amri kumi za Mungu.Swali la kujiuliza hapa je jirani yangu ni nani? Jibu ni kwamba jirani ni mtu yeyote aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu hata wale tunao wadhania kuwa ni adui zetu  pia ni jirani zetu.

Tunaelezwa majadiliano kati yaYesu na mwalimu wa sheria,kuhusu amri gani iliyo kuu kwani hapo mwanzo Wayahudi hawakuchangamana na watu wa mataifa mengine Mfano: Myahudi na Msamaria, kwani Wayahudi walijiona kuwa watu wa tabaka la juu watu walio staharabika, hivyo haikuwa rahisi kwao kujichanganya na Wasamaria kwani Wasamaria walionekana kuwa watu duni wa tabaka la chini  kati hadhi zote za utu.Ndipo Yesu anamweleza wazi wazi kwamba amri iliyo kuu ni amri ya mapendo kwa Mungu na jirani.(Marko 12:31).Lengo la yesu kutoa amri kuu ni kwamba kuondoa matabaka kati ya Myahudi na Msaamria. Mama Theresa wa Calcuta anaendelea kusema “penye upendo pana maisha”. Leo hii swali la kujiuliza je mimi na wewe tunatimiza je amri hii kuu ya mapendo kwa Mungu na jirani? ,je upendo wetu umelenga nini hasa?,je tunawajibika kikamilifu katika wajibu zetu kama wewe ni kiongozi, Baba  nawe Mama, wewe mtoto, wewe kijana je unawajibika je katika jumuiya yako na jamii inayo kuzunguka?

         Sifa za upendo wa kweli ni hizi , Upendo huvumilia, hufadhili, haujivuni, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya, haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na ukweli (1Kor 13:4-6). Mtakatifu Papa Yohane Paulo wa II naye aliwahi kusema “tunatakiwa kumpenda Yesu Kristo katika jirani zetu ,tukishindwa kumpenda Kristo katika jirani zetu  utashindwa kuishi ukristo na huwezi kusema wewe ni mkristo”. Hivyo ndugu katika Kristo swali la kujiuliza mimi na wewe je kweli upendo kwa Mungu na jirani tunao? na kama upo kweli je ni ule anaousisitiza Yesu Kristo?. Upendo kwa Mungu na jirani utajidhihirisha wazi kulingana na huduma zetu katika famiia zetu,jumuiya zetu na jamii nzima inayotuzunguka katika walio wahitaji kama alivyonyesha upendo Yule msamaria kwa Yule aliyejeruhiwa.Upendo wa Mungu na jirani utaonekana tu pale tukatapo timiza wajibu zetu kikamiifu kwa kijitoa kwa dhati kwa ajii ya wengine.

TAFAKARI HII IMETOLEWA NA MIMI FRT. JOACHIM TUMAINI

WA JIMBO KATOLIKI SINGIDA

MWAKA WA KWANZA THEOLOGIA, SEMINARY KUU YA MTAKATIFU PAULO MTUME KIPALAPALA- JIMBO KUU LA TABORA

 

Bikira Maria Malkia wa Mitume…..Utuombee

 

FRT. JOACHIM TUMAINI

JIMBO KATOLIKI SINGIDA

 

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.